Ni ipi hukumu ya kufunga siku ya ´Arafah kwa wasiokuwa mahujaji na mahujaji?

Swali: Ni ipi hukumu ya kufunga siku ya ´Arafah kwa wasiokuwa mahujaji na mahujaji?

Jibu: Kufunga siku ya ´Arafah kwa ambao si mahujaji ni Sunnah iliokokotezwa. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu kufunga siku ya ´Arafah:

“Nataraji kutoka kwa Allaah anisamehe mwaka wa kabla yake na mwaka wa baada yake.”

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Nataraji kutoka kwa Allaah anisamehe mwaka uliopita na unaokuja.”

Kuhusu kufunga wale ambao ni mahujaji si Sunnah kwao kufunga siku ya ´Arafah. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa si mwenye kufunga siku ya ´Arafah katika hajj ya kuaga. Katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy kupitia kwa Maymuunah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ya kuwa watu walikuwa na mashaka kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefunga siku ya ´Arafah ambapo nikamuagizia maziwa naye amesimama kiwanjani ambapo akanywa na huku watu wanamtazama.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawa (20/47)
  • Imechapishwa: 13/08/2018