Swali: Ni yepi yenu kuhusu tiba inayoua hamu ya jimaa? Nimesikia kuhusu tiba inayoitwa kafuri. Ni yepi maoni yenu kuhusu hilo?
Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu shida ya nguvu ya matamanio na khatari yake:
“Enyi kongamano la barobaro! Yule atakayeweza miongoni mwenu kuoa basi na aoe. Hakika hilo linamfanya ainamishe macho na inahifadhi utupu wake. Yule asiyeweza basi ni juu yake afunge. Kwani kwake ni kinga.”[1]
Hivyo inafaa kwako kufunga kwa kadiri inavyowezekana, kutegemea msaada wa Allaah, kisha kwa kufunga ambako Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekuelekeza ikiwa unaweza kufanya hivyo. Na kama huwezi, basi wasiliana na madaktari waliobobea katika jambo hili ili wakuelekeze katika mambo yatakayokusaidia kujihifadhi na kujizuia na matamanio yaliyoharamishwa na Allaah.
Kuna dawa zinazodhoofisha shahwa, haziondoi kabisa, bali zinaipeleka katika udhaifu mpaka zipatikane sababu halali za kuikidhi. Hivyo unatakiwa kuwauliza wataalamu wenye ujuzi katika jambo hili ili wakuelekeze katika sababu zitakazokusaidia kuizuia shahwa yako na kujilinda dhidi ya kuvuka mipaka yake, kwa kutumia dawa zinazofaa ambazo haziikati kabisa wala haziwezi kukudhuru, bali zinaipeleka katika udhaifu kwa muda maalum tu mpaka Allaah akuwezeshe ndoa na kuikidhi katika halali. Na kufunga, endapo utaweza, ndilo tiba bora na yenye faida zaidi ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameielekeza.
Kuna jambo muhimu pia la kufahamika, nalo ni ndoa ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameielekeza. Vijana wengi wanapuuza ndoa na kuiacha. Mara nyingine wanahimizwa na wenzao kuacha, mara wakaambiwa wasubiri mpaka masomo yaishe, mara mpaka apate kazi, mara mpaka kitu fulani na mengineyo, jambo ambalo ni kosa. Ni wajibu kuharakisha ndoa pale inapowezekana, hata kama kupitia baba yako, kaka yako mkubwa, mama yako au njia yoyote ile unayoweza kupata ndoa. Harakisha ndoa na usisubiri mpaka masomo yaishe, kazi, nyumba ya kumiliki wala udhuru mwingine. Harakisha ndoa. Aliyeoa Allaah atamsaidia. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَأَنكِحُوا الْأَيَامَىٰ مِنكُمْ وَالصَّالِحِينَ مِنْ عِبَادِكُمْ وَإِمَائِكُمْ ۚ إِن يَكُونُوا فُقَرَاءَ يُغْنِهِمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ
“Waozesheni wajane miongoni mwenu na walio wema kati ya watumwa wenu wanaume na wajakazi wenu. Wakiwa mafakiri Allaah basi Atawatajirisha katika fadhila Zake.”[2]
Hivyo ndoa ikafanywa ni miongoni mwa sababu za kupata utajiri.
Kwa hiyo lazimiana na ndoa na iharakishe. Usicheleweshe mpaka masomo yaishe au sababu nyinginezo. Bali inapowezekana, hata kupitia baba yako, kaka, mama au njia yoyote, basi usicheleweshe. Bali harakisha na fanya bidii. Kwa kuwa katika ndoa kuna manufaa mengi, kama vile:
1 – Kushusha macho chini.
2 – Kuhifadhi tupu.
3 – Kuongeza kizazi na kukithirisha ummah.
4 – Allaah atakutajirisha na kukusaidia kwa manufaa mengi.
Inatambulika pia kwamba ndoa inaleta utulivu wa nafsi, hifadhi ya moyo na raha. Allaah amewafanya wake kuwa ni utulivu kwa waume zao:
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا
“Miongoni mwa alama Zake ni kwamba amekuumbieni katika jinsi yenu wake ili mpate utulivu kwao.”[3]
Kwa hiyo wake wamefanywa na Allaah kuwa ni utulivu, faraja na raha kwa waume zao. Mtu anapooa, basi anakuwa amepata msaada kwa kitu ambacho Allaah amekifanya kuwa ni faraja na utulivu wa moyo. Basi usicheleweshe jambo hili ambalo Allaah amekufanyia kuwa ni faraja na msaada katika wema na kinga dhidi ya yale aliyoyaharamisha Allaah.
[1] al-Bukhaariy na Muslim.
[2] 24:32
[3] 30:21
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2810/ما-حكم-العلاج-الذي-يخفف-من-شدة-الشهوة
- Imechapishwa: 02/09/2025

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2810/ما-حكم-العلاج-الذي-يخفف-من-شدة-الشهوة
Imechapishwa: 02/09/2025
https://firqatunnajia.com/ni-ipi-hukumu-ya-dawa-zinazopunguza-au-kuondosha-hamu-ya-jimaa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket