Ni ipi hukumu ya ambaye anamuogopa mtu?

Swali: Ni ipi hukumu ya ambaye anamuogopa mtu?

Jibu: Ikiwa ana sababu ya kufanya hivo. Kwa mfano anamuogopa mfalme mwenye kudhulumu au anaogopa asikutane na mtu njiani na hivyo akachukua silaha na kujitenga mbali na sababu za shari. Ikiwa khofu ina sababu hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 31
  • Imechapishwa: 10/06/2019