Swali: Nini afanye ambaye anafanya hajj akichelewa kutoka ´Arafah kutokana na msongamano mkubwa na akakhofia kutoka wakati wa ´Ishaa kabla ya kufika Muzdalifah?
Jibu: Akikhofia kutoka kwa wakati, basi atalazimika kushuka na kuswali. Baadhi ya mahujaji hawaswali Maghrib na ´Ishaa mpaka wafike Muzdalifah ijapo umekwishatoka wakati wa swalah ya ´Ishaa. Kitendo hicho hakijuzu. Ni haramu na ni dhambi kubwa. Kwa mujibu wa dalili ya Qur-aan na Sunnah ni haramu kuchelewesha swalah mpaka ukatoka wakati wake. Allaah (Ta´ala) amesema:
إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا
“Kwani hakika swalah kwa waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalum.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amebainisha na kuzipanga nyakati hizi. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّـهِ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ
”Hiyo ndio mipaka ya Allaah; na yeyote atakayevuka mipaka ya Allaah, basi kwa hakika ameidhulumu nafsi yake.”[2]
تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ فَلَا تَعْتَدُوهَا ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ
”Hiyo ni mipaka ya Allaah, hivyo basi msivuke mipaka; yeyote atakayevuka mipaka ya Allaah basi hao ndio madhalimu.”[3]
[1] 04:103
[2] 65:1
[3] 2:229
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/205-206)
- Imechapishwa: 15/04/2026
Swali: Nini afanye ambaye anafanya hajj akichelewa kutoka ´Arafah kutokana na msongamano mkubwa na akakhofia kutoka wakati wa ´Ishaa kabla ya kufika Muzdalifah?
Jibu: Akikhofia kutoka kwa wakati, basi atalazimika kushuka na kuswali. Baadhi ya mahujaji hawaswali Maghrib na ´Ishaa mpaka wafike Muzdalifah ijapo umekwishatoka wakati wa swalah ya ´Ishaa. Kitendo hicho hakijuzu. Ni haramu na ni dhambi kubwa. Kwa mujibu wa dalili ya Qur-aan na Sunnah ni haramu kuchelewesha swalah mpaka ukatoka wakati wake. Allaah (Ta´ala) amesema:
إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا
“Kwani hakika swalah kwa waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalum.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amebainisha na kuzipanga nyakati hizi. Allaah (Ta´ala) amesema:
وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّـهِ فَقَدْ ظَلَمَ نَفْسَهُ
”Hiyo ndio mipaka ya Allaah; na yeyote atakayevuka mipaka ya Allaah, basi kwa hakika ameidhulumu nafsi yake.”[2]
تِلْكَ حُدُودُ اللَّـهِ فَلَا تَعْتَدُوهَا ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ اللَّـهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ
”Hiyo ni mipaka ya Allaah, hivyo basi msivuke mipaka; yeyote atakayevuka mipaka ya Allaah basi hao ndio madhalimu.”[3]
[1] 04:103
[2] 65:1
[3] 2:229
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/205-206)
Imechapishwa: 15/04/2026
https://firqatunnajia.com/ni-haramu-kuichelewesha-swalah-mpaka-ukatoka-wakati-wake/