Swali: Je, swalah kwa kuelekea makaburi ni batili?

Jibu: Ndio, batili, batili na zaidi ya hivo.

Swali: Vipi kuhusu kuswali kando ya njia?

Jibu: Kumepokelewa Hadiyth hii ambayo ni dhaifu. Bora ni kuepuka kufanya hivo. Kumepokelewa katika baadhi ya mapokezi mengine kuepuka… kando ya njia, kwa sababu ni kimbilo la wanyama waharibifu. Bora ni kuepuka kukaa na kuswali, kwa sababu ni jambo la khatari.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24824/حكم-الصلاة-الى-القبور-وفي-قارعة-الطريق
  • Imechapishwa: 15/12/2024