ar-Raajihiy: Anayevaa nguo yake chini ya kongo mbili za mguu jambo lake halitoki kati ya kubwa kiasi fulani au dhambi kubwa kabisa, kama ambaye anaburuta nguo yake kwa kiburi?

Ibn Baaz: Madhambi makubwa yanatofautiana. Madhambi makubwa yenyewe yanatofautiana.

ar-Raajihiy: Katika hali zote mbili ni dhambi kubwa?

Ibn Baaz: Ndio, ndio udhahiri wa dalili. Mwanamke anayeombolewa ni dhambi kubwa, uzinzi ni dhambi kubwa zaidi kuliko ya kwanza, kuwaasi wazazi wawili ni dhambi kubwa, kuwakata ndugu ni dhambi nyingine kubwa. Hata hivyo kuwakata wasiokuwa wazazi wawili ni jepesi kidogo kuliko kuwaasi na kuwakata wazazi wawili. Madhambi makubwa yanatofautiana kama ambavo madhambi madogo pia yanatofautiana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24809/هل-تتفاوت-كباىر-الذنوب-وصغاىرها
  • Imechapishwa: 17/12/2024