Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hazini mwenye kuzini pale anapozini hali ya kuwa ni muumini, hanywi pombe mwenye kunywa pombe pale anapokunywa hali ya kuwa ni muumini na wala hapori kitu, jambo linalofanya watu kumuinulia macho, hali ya kuwa ni muumini.”[1]

Pombe ni yale yote yanayoidumaza akili, ni mamoja kinatokana na kinywaji, vidonge au kitu kingine. Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kila chenye kulewesha ni pombe na kila pombe ni haramu.”[2]

Chapombe anayekufa huku bado anakunywa pombe hatokunywa pombe huko Peponi. Ni neema kutoka kwa Allaah ambayo unalipwa thawabu kwayo kwa kule kuicha na wakati huohuo huna utambuzi nayo. Unaona pombe ndani ya chupa na hujui kama ni pombe unayoona. Kama tulivosema ni neema kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ambayo unalipwa thawabu kwayo kwa kule kuiepuka na wakati huohuo wala hata huitamani.

[1] al-Bukhaariy (2475) na Muslim (57).

[2] Muslim.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 259-260
  • Imechapishwa: 13/04/2025