Swali: Imetajwa katika ”ar-Radhw” ya kwamba inajuzu kutoa zakaah kuwapa ndugu wa karibu hata kama wanakurithisha iwapo hauwajibiki kuwahudumia?
Jibu: Haya ni maoni yanayotambulika vyema. Ikiwa mtu halazimiki kuwahudumia, basi anaweza kuwapa zakaah. Kama anawarithi, bado asiwape. Bali anawapa wale ambao hawamrithi. Hata hivyo maoni haya yanahitaji kuangaliwa vyema. Maoni sahihi ni kwamba hakuna kosa kutoa zakaah kwa ndugu wa karibu masikini kwa ujumla, hata kama mtu anawarithi iwapo watakufa. Maoni sahihi ni kwamba hukumu haijahusishwa na suala la kurithi, bali imejengwa juu ya ufukara na uhitaji. Hivyo basi ndugu wa karibu wakiwa wahitaji, basi wanapewa zakaah. Hiyo inakuwa ni swadaqah na kuunga undugu, isipokuwa kwa mzazi na mtoto. Wazazi na mababu (upande wa juu) na watoto na wajukuu (upande wa chini). Ibn-ul-Mundhir amepokea maafikiano ya kuwa mzazi na mtoto hawapeani zakaah. Wazazi, mama, mababu, mabibi, watoto na wajuku, hawa hawapewi zakaah. Bali ndugu yao mwenye uwezo anawajibika kuwahudumia kadiri ya uwezo wake. Ama kaka, dada, ami, shangazi, mjomba, mama mdogo na watoto wa, hawa wanapewa zakaah bila kikomo kwa mujibu wa maoni sahihi, iwapo ni masikini.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1022/مشروعية-دفع-الزكاة-للاقارب
- Imechapishwa: 09/01/2026
Swali: Imetajwa katika ”ar-Radhw” ya kwamba inajuzu kutoa zakaah kuwapa ndugu wa karibu hata kama wanakurithisha iwapo hauwajibiki kuwahudumia?
Jibu: Haya ni maoni yanayotambulika vyema. Ikiwa mtu halazimiki kuwahudumia, basi anaweza kuwapa zakaah. Kama anawarithi, bado asiwape. Bali anawapa wale ambao hawamrithi. Hata hivyo maoni haya yanahitaji kuangaliwa vyema. Maoni sahihi ni kwamba hakuna kosa kutoa zakaah kwa ndugu wa karibu masikini kwa ujumla, hata kama mtu anawarithi iwapo watakufa. Maoni sahihi ni kwamba hukumu haijahusishwa na suala la kurithi, bali imejengwa juu ya ufukara na uhitaji. Hivyo basi ndugu wa karibu wakiwa wahitaji, basi wanapewa zakaah. Hiyo inakuwa ni swadaqah na kuunga undugu, isipokuwa kwa mzazi na mtoto. Wazazi na mababu (upande wa juu) na watoto na wajukuu (upande wa chini). Ibn-ul-Mundhir amepokea maafikiano ya kuwa mzazi na mtoto hawapeani zakaah. Wazazi, mama, mababu, mabibi, watoto na wajuku, hawa hawapewi zakaah. Bali ndugu yao mwenye uwezo anawajibika kuwahudumia kadiri ya uwezo wake. Ama kaka, dada, ami, shangazi, mjomba, mama mdogo na watoto wa, hawa wanapewa zakaah bila kikomo kwa mujibu wa maoni sahihi, iwapo ni masikini.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1022/مشروعية-دفع-الزكاة-للاقارب
Imechapishwa: 09/01/2026
https://firqatunnajia.com/ndugu-wanaopewa-na-wasiopewa-zakaah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket