Ndugu waliyo khatari zaidi kuliko maradhi ya ngozi unaopaswa kuwaepuka

Swali: Hakika Hijrah ina milango na sehemu nyingi sana, miongoni mwazo ni Hijrah ya dola, na ya watu binafsi na wengine. Basi swali ni kwamba mimi ni mtu ninaishi katika mazingira ambayo ndani yake kuna maovu yote. Katika mazingira haya kuna watu wasiojua swalah. Kipi kinachonipasa? Je, niache nyumba hii au nifanye nini?

Jibu: Ndiyo, usiishi miongoni mwa familia ovu iliyo kinyume na Uislamu, isiyojua swalah na inayoridhia maovu. Usiishi miongoni mwao. Wakimbie. Lakini hilo lisikuzuie kufanya ulinganizi. Waite kwa Allaah, wanasihe, waongoze na wewe huku ukiwa mbali na kuishi pamoja nao ili wasikudhuru na ili wasikuvute kwenda kwao. Wao ni khatari zaidi kuliko maradhi ya ngozi. Ni khatari zaidi kuliko maradhi ya ngozi. Kwa hiyo jihadhari nao. Lakini hilo lisikuzuie kutoa nasaha, maelekezo na uongofu kwa maandishi au kwa maneno unapoweza kuwanasihi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2187/حكم-معايشة-اشخاص-لا-يحافظون-على-الصلاة
  • Imechapishwa: 31/05/2026