Kusoma Basmalah kwa sauti inafaa ingawa bora ni kutofanya hivo

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu anayesoma Basmalah kwa sauti ya juu katika kisomo cha al-Faatihah kwa makusudi katika Maghrib, ´Ishaa na Fajr?

Jibu: Hana kosa, lakini kuacha kufanya hivyo ni bora zaidi. Sunnah na lililo bora ni asisome Basmalah kwa sauti ya juu. Anayelisoma kwa sauti ya juu hana tatizo lolote ikiwa amefanya hivyo kwa Ijtihaad yake au kwa kumuiga mwanachuoni anayemfuata. Lakini ameacha lililo bora na ameacha Sunnah iliyoenea na inayojulikana. Kilicho bora kwake na kinachopendelewa ni asilisome Basmalah kwa sauti ya juu, kwa kuwa lililothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kutoka kwa Maswahabah wake wawili Abu Bakr as-Swiddiyq na ´Umar na pia kutoka kwa ´Uthmaan ni kutosoma ”Bismillaah ar-Rahmaan ar-Rahiym” kwa sauti ya juu. Imepokelewa kutoka kwa baadhi ya Maswahabah kama Abu Hurayrah na wengineo ya kwamba aliisoma kwa sauti ya juu. Kwa hivyo mwenye kuisoma kwa sauti ya juu hapana vibaya, lakini ameacha lililo bora na lililopendelewa kufanywa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2218/الجهر-بالبسملة-عند-قراءة-الفاتحة
  • Imechapishwa: 31/05/2026