Swali: Je, mwimbaji huhesabiwa kuwa ni miongoni mwa askari wa Ibliys? Je, ushahidi wake hukubaliwa? Je, muislamu atahesabiwa iwapo atamwambia mtu mtenda maasi au fasiki ”Wewe ni mmoja wa askari wa Ibliys” au ”Wewe ni shaytwaan”?

Jibu: Kila anayelingania uovu ni miongoni mwa askari wa Ibliys. Ibliys ana askari. Kila anayelingania maasi, ni mamoja iwe kwa Bid´ah, kwa nyimbo, kwa kwa maneno yasiyo nyimbo, kwa hotuba au kwa mengineyo, kila anayelingania Bid´ah, shirki au maasi miongoni mwa waimbaji, wapigaji wa ala, wazushi, wanaolingania uzinzi, kamari na maasi, wote hao ni askari wa shaytwaan. Askari wa shaytwaan ni wanaolingania uharibifu. Askari wa Allaah ni wanaolingania haki na uongofu. Hivyo basi anayelingania haki kwa matendo yake au kwa maneno yake, huyo ni miongoni mwa kundi na askari wa Allaah. Anayelingania maasi, Bid´ah na shirki kwa nyimbo, kwa maneno mengine, kwa hotuba, kwa maandishi au kwa mengineyo, huyo ni miongoni mwa askari wa shaytwaan.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2214/الدعاة-الى-المعاصي-من-جنود-ابليس
  • Imechapishwa: 31/05/2026