Swali: Kuna mwanamke amezikwa kwa mujibu wa Sunnah. Baada ya hapo mvulana wake akaota namna ambavyo mama yake anamlaumu kwa kumvulia adabu na kwa sababu hakujenga juu ya kaburi lake ambapo mtoto huyu akawa amejenga juu ya kaburi la mama yake. Je, ndoto kama hizi zitendewe kazi au zinatokamana na shaytwaan?

Jibu: Zinatokamana na shaytwaan. Asizingatie ndoto hizi na wala asiitendee kazi. Inaenda kinyume na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (43) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2019%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020