Swali: Mwanaume alizini na mwanamke, akabeba mimba ya haramu, kisha akaenda kwa baba yake, akaomba kumuoa na baadaye wakaoana hali mwanamke ana mimba ya miezi mitatu. Ni ipi hukumu ya ndoa hii? Ni kipi kiwango cha kusihi kwa ndoa hii? Je, watoto wao ni wenye kukubalika kwa mujibu wa Shari´ah au hapana?
Jibu: Ndoa haisihi pamoja na mimba ya zinaa mpaka watubu, mpaka amalize ada ya zinaa hii iliyoharibika, mpaka ajitakase kwa kupata hedhi moja na atubu, kisha baada ya hapo aolewe.
Mwanafunzi: Hata kama mimba ni yake?
Ibn Baaz: Hata kama ni yake, kwa sababu mimba hii haimhusu. Ni uzinzi. Mtoto hanasibishwi kwake. Kisha mwanamke mzinifu ni lazima atakiwe kutubu. Hukumu hiyohiyo inamuhusu mwanaume, kwa sababu haifai amuoe isipokuwa baada ya kudhihiri tawbah kwake. Yeye pia mwanamme si mwenye kufaa mpaka idhihiri tawbah kwake. Hivyo kwa hali yoyote ni kwamba wote wawili wanapaswa kutakiwa kutubia.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1464/حكم-نكاح-الزاني-بمن-زنى-معها-حال-حملها
- Imechapishwa: 20/12/2025
Swali: Mwanaume alizini na mwanamke, akabeba mimba ya haramu, kisha akaenda kwa baba yake, akaomba kumuoa na baadaye wakaoana hali mwanamke ana mimba ya miezi mitatu. Ni ipi hukumu ya ndoa hii? Ni kipi kiwango cha kusihi kwa ndoa hii? Je, watoto wao ni wenye kukubalika kwa mujibu wa Shari´ah au hapana?
Jibu: Ndoa haisihi pamoja na mimba ya zinaa mpaka watubu, mpaka amalize ada ya zinaa hii iliyoharibika, mpaka ajitakase kwa kupata hedhi moja na atubu, kisha baada ya hapo aolewe.
Mwanafunzi: Hata kama mimba ni yake?
Ibn Baaz: Hata kama ni yake, kwa sababu mimba hii haimhusu. Ni uzinzi. Mtoto hanasibishwi kwake. Kisha mwanamke mzinifu ni lazima atakiwe kutubu. Hukumu hiyohiyo inamuhusu mwanaume, kwa sababu haifai amuoe isipokuwa baada ya kudhihiri tawbah kwake. Yeye pia mwanamme si mwenye kufaa mpaka idhihiri tawbah kwake. Hivyo kwa hali yoyote ni kwamba wote wawili wanapaswa kutakiwa kutubia.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1464/حكم-نكاح-الزاني-بمن-زنى-معها-حال-حملها
Imechapishwa: 20/12/2025
https://firqatunnajia.com/ndoa-ya-mwanaume-kumuoa-aliyemzini/