Ndoa wakati wa ujauzito baada ya kuzini

Swali: Mwanaume akizini na mwanamke kisha akashika mimba na baada ya hapo akamuoa kipindi cha ujauzito wake. Je, mtoto huyu anahesabiwa ni wa kwake au anahesabiwa ni mtoto wa uzinzi?

Jibu: Ni mtoto wa nje ya ndoa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mtoto ni wa kitandani na mzinzi analo jiwe.”

Hiyo maana yake ni kwamba mtoto anamfuata mama yake na anazingatiwa kuwa ni mtoto wa nje ya ndoa. Kusema kwamba mzinzi analo jiwe maana yake ni kwamba ana khasara, majuto na hana jengine.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 297
  • Imechapishwa: 01/08/2025