Swali: Ni yapi maoni yako kwa mwenye kusema kuwa haitakikani kuwafunza vijana wenye msimamo mfumo [Manhaj] kwa kuwa hili linawasababishia kuangamia. Ni bora kwa kijana kuwa Tabliygh au Ikhwaaniy kuliko kuangamia kwa kufunzwa mfumo.

Jibu: Ni kuangamia kwa sampuli gani huku? Ni kuritadi? Kusoma mfumo wa Salaf-us-Swaalih mtu anakuwa mwenye kuritadi? Mambo ni kama mnavyoona Jamaa´at-ut-Tabliygh na al-Ikhwaan al-Muslimuun ni watu wa Bid´ah na huyu anayesoma mfumo anakuwa ni mbaya zaidi kuliko wao! Je, anakuwa kafiri au anakuwa vipi?

Linalojulikana kwa mujibu wa Ahl-us-Sunnah ni kwamba mtenda madhambi ni mwenye shari kidogo na sahali kuliko mtu wa Bid´ah. Mtu ambaye ni mtenda dhambi lakini wakati huo huo ni Ahl-us-Sunnah, bi maana anaitakidi I´tiqaad sahihi, anaamini na kuheshimu mfumo huu, lakini hata hivyo matamanio yamemzidi – hata kama ni kweli kuwa ni Faasiq na muasi – lakini hata hivyo yuko chini kuliko mtu wa Bid´ah anayeonelea kuwa mfumo huu si sahihi na ni batili na akawa anaupiga vita. Haijalishi kitu sawa ikiwa ni Tabliygh au Ikhwaan. Hawa ni waovu zaidi kuliko watenda madhambi.

Mtu anayeamini mfumo wa Salaf ndio haki, wako katika haki na anawapenda watu wenye mfumo huu, lakini akawa amepinda katika tabia yake, mwenendo wake na kadhalika. Mwingine anaamini kuwa watu wenye mfumo huu ni batili, anawapiga vita Waislamu, Tawhiyd na watu wenye mfumo huu. Anaswali na kumuabudu Allaah usiku na mchana. ´Ibaadah hizi zina uzito upi?

Mwenye kusema hivi ni mjinga na adui wa mfumo huu.

Mfumo huu ndio sababu ya mtu kuwa na msimamo na uthabiti – Allaah akitaka. Yule ambaye Allaah Anamtakia kheri hujifunza mfumo huu na akawa na msimamo mkamilifu katika ´Aqiydah yake, mfumo wake na tabia yake.

Ina maana aende kusoma mfumo wa Tabliygh ulio na Huluul, Wahdat-ul-Wujuud, ukhurafi na pumba! Hapana.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=26897
  • Imechapishwa: 20/05/2015