Swali: Pote la Ibaadhiyyah na Ismaa´iliyyah wanathibitisha sifa za Allaah au wanazikanusha?

Jibu: Ibaadhiyyah ni pote katika Khawaarij. Wanafuata mfumo wa Mu´tazilah ambapo wanakanusha sifa za Allaah.

Kuhusu Ismaa´iliyyah ni katika Faatwimiyyah. Hawa ni wabaya zaidi. Wana dini ya kipekee. Hawa wanasema kuwa dini ina [maana ya] undani na ya uinje. Haihusiani na masuala ya sifa za Allaah. Wana jambo kubwa kuzidi haya ya sifa. Hawa wana dini yao ya kipekee. Wanasema kuwa kuna mambo ya dini ya undani. Ismaa´iliyyah ni Baatwiniyyah. Kwanza wanapinga kufufuliwa, kutolewa ndani ya makaburi, Pepo na Moto. Wanasema kuwa vyote hivi havina uhakika. Waliyoelezea Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim was-Salaam) ni kuwadanganya watu. Waliwadanganya watu ili waweze kuishi vizuri. Uhakika wa mambo hakuna Pepo wala Moto, ndivyo wanavyosema. Wanasema kuwa kuna maana ya uinje na ya undani ya swalah. Maana ya uinje ya swalah ni zile swalah tano wanazoswali waislamu. Maana ya swalah ya undani ni kujua zile siri za wanachuoni wao. Kadhalika swawm ina maana ya undani na ya uinje. Maana ya uinje ni ile swawm wanayofunga waislamu ambapo wanajizuia na vile vitu vyeye kufunguza kuanzia pale alfajiri inapoingia mpaka jua linapozama. Maana ya swawm ya undani ni kuficha siri za wanachuoni wao. Hajj ina maana ya uinje na ya undani. Maana yake ya uinje ni ile hajj inayofanywa na waislamu kwenda kuitembelea nyumba ya Allaah tukufu. Wanasema kuwa hii ndio hajj ya wasiokuwa wasomi. Maana ya hajj ya wasomi ni kufunga safari kwenda kwa wanachuoni wao. Hii ni dini ya kipekee. Hawa ndio Baatwiniyyah. Shaykh-ul-Islaam amesema kuhusu Baatwiniyyah:

“Wameafikiana waislamu juu ya kwamba watu hawa ni makafiri zaidi kuliko mayahudi na manaswara.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qaa´idah al-Marraakushiyyah (03)
  • Imechapishwa: 30/04/2020