Ndio maana al-Fawzaan anafupiza wakati wa kujibu maswali

Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Uislamu ni kushuhudia kuwa hapana mola anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Mtume wa Allaah, kusimamisha Swalah, kutoa Zakaah, kufunga Ramadhaan na kwenda kuhiji ukiweza.”  Akasema: “Umesema kweli!” Tukashangazwa kwa kumuuliza kwake Mtume na kumsadikisha. 

MAELEZO

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Uislamu ni kushuhudia kuwa hapana mola anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Mtume wa Allaah, kusimamisha Swalah, kutoa Zakaah, kufunga Ramadhaan na kwenda kuhiji ukiweza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimweleza nguzo za Uislamu ambazo ni lazima. Nguzo hizi zikihakikika na kupatikana basi Uislamu umehakikiwa. Ama mambo mengine yenye kuzidi juu yake ni yenye kukamilisha tu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifupika na kubainisha nguzo za Uislamu. Namna ambavyo jibu litakuwa ni fupi ndivyo itavokuwa rahisi kwa yule mwenye kujifunza na yule mwenye kusikiliza. Inakuwa ni sahali kwake kulihifadhi na kulielewa. Upande mwingine jibu likiwa refu zaidi inakuwa ni vigumu kwa wale wafuatiliaji. Jengine ni kwamba huenda wengi wasilielewe. Hii ni dalili inayoonyesha kwamba yule muulizwaji anatakiwa kuzingatia suala la kufupisha kiasi atavyoweza. Afupize juu ya kitu cha kilazima. Vinginevyo Uislamu una mengi zaidi ya hayo. Hizi ndio nguzo zake ambazo umesimama juu yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 186
  • Imechapishwa: 12/03/2019