Swali: Je, inajuzu kwa muumini kusema ”Mimi ni muumini – Allaah akitaka”?
Jibu: Ndio, inajuzu kwa mujibu wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kwa mtu kusema Mimi ni muumini – Allaah akitaka”. Makusudio ya kusema hivo siyo shaka katika imani yake. Bali maana yake ni kwa kuzingatia kwamba hajui kama amekamilisha imani yake ipasavyo au hapana. Imani ina mambo ya wajibu na ina mambo yanayohusiana na kuacha yaliyoharamishwa. Kwa hiyo anaposema hivo, anakusudia imani yangu iwe kamili – kwa idhini ya Allaah – au kwa kuzingatia mwisho wake, kwa sababu hajui atahitimishwa vipi.
Kuhusu Murji´ah wanakanusha kusema hivyo na wakidai kuwa ni shaka, jambo ambalo ni makosa. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah husema hivo katika imani bila shaka yoyote, bali kwa kuzingatia ukamilifu wa wajibu wa imani na kwa kuzingatia atamalizia vipi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1532/حكم-الاستثناء-في-الايمان
- Imechapishwa: 27/03/2026
Swali: Je, inajuzu kwa muumini kusema ”Mimi ni muumini – Allaah akitaka”?
Jibu: Ndio, inajuzu kwa mujibu wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kwa mtu kusema Mimi ni muumini – Allaah akitaka”. Makusudio ya kusema hivo siyo shaka katika imani yake. Bali maana yake ni kwa kuzingatia kwamba hajui kama amekamilisha imani yake ipasavyo au hapana. Imani ina mambo ya wajibu na ina mambo yanayohusiana na kuacha yaliyoharamishwa. Kwa hiyo anaposema hivo, anakusudia imani yangu iwe kamili – kwa idhini ya Allaah – au kwa kuzingatia mwisho wake, kwa sababu hajui atahitimishwa vipi.
Kuhusu Murji´ah wanakanusha kusema hivyo na wakidai kuwa ni shaka, jambo ambalo ni makosa. Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah husema hivo katika imani bila shaka yoyote, bali kwa kuzingatia ukamilifu wa wajibu wa imani na kwa kuzingatia atamalizia vipi.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1532/حكم-الاستثناء-في-الايمان
Imechapishwa: 27/03/2026
https://firqatunnajia.com/ndio-maana-ahl-us-sunnah-wakafanya-uvuaji-katika-imani/