Nchi ya Kiislamu au isiyo ya Kiislamu? – inategemea na zile alama zinazodhihiri zaidi

Swali: Kuhusu nchi za kiislamu, nyingi kati yao zina matendo ya ushirikina na kuna majengo wanayosema kuwa ni ya watu wema na kadhalika. Je, nchi hizi zinaitwa za Kiislamu au zisizo za Kiislamu?

Jibu: Hili ni jambo linahitaji kuangaliwa vyema. Ikiwa alama za ukafiri ndizo zinazoonekana zaidi katika nchi hiyo, basi ni nchi ya kikafiri. Na ikiwa alama za Uislamu ndizo zinazoonekana zaidi na ndizo zinazotawala, basi ni nchi ya Kiislamu. Hali inazingatiwa kulingana na kile kinachoonekana kwa uwazi na kilicho na nguvu zaidi ndani ya nchi hiyo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25418/هل-البلاد-التي-بها-ممارسات-شركية-تسمى-اسلامية
  • Imechapishwa: 23/03/2025