Swali: Mimi ni mwanamke nina mume na watoto watano, lakini mume wangu ameoa mwanamke mwingine ambaye anamtilia umuhimu zaidi kuliko mimi na watoto wangu na hunizuia mambo ambayo anamruhusu mwanamke mwingine. Hali yangu naye iko hivi. Unasemaje juu ya hilo?
Jibu: Wajibu juu ya mume ni kufanya uadilifu baina ya wake zake na wala haruhusiwi kudhulumu. Yeye ataulizwa juu ya jambo hili. Hivyo ni wajibu kwa wanaume waliooa wake zaidi ya mmoja kufanya uadilifu baina yao, wamtake msaada Allaah na wamchunge (Subhaanahu wa Ta´ala) katika kila jambo: katika kugawa zamu, katika matumizi na katika mambo ya kuwatuliza nyoyo zao na kuepuka kueneza chuki baina yao. Hivi ndivyo inavyopaswa kwa mume kuwa na hekima, ajitahidi kwa kila jambo linalotuliza hali na kurekebisha nyoyo, kuwafanya wake wawili au zaidi wawe katika raha na utulivu kwa sababu ya uadilifu wake, uangalizi wake na tabia yake njema kwao wote. Huu ndio wajibu wake.
Tunawanasihi wake pia wasaemehe baadhi ya mambo, wasiwe wakali sana na wasichunguze kila jambo. Kwa sababu mwenye kufanya ugumu atajuta na ugumu huo unaweza kuvunja familia na maisha ya ndoa isipokuwa Allaah atakavyo. Hivyo inafaa kwa wanawake pia kusamehe baadhi ya mambo na wasimkaze sana mume katika masuala ya uadilifu ikiwa ni makosa madogo au jambo dogo, kwani yanahitaji kuvumiliwa na kupuuzwa. Lazima kuwe na juhudi kutoka kwa mume na pia msamaha kutoka kwa wake katika baadhi ya mambo yanayoweza kutokea kutoka kwa mume, huenda si kwa makusudi au huenda amelazimika nayo. Basi inafaa kwa mwanamke kumsamehe baadhi ya mambo ili ipatikane maelewano na ushirikiano katika kheri.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3377/العدل-بين-الزوجات
- Imechapishwa: 21/09/2026
Swali: Mimi ni mwanamke nina mume na watoto watano, lakini mume wangu ameoa mwanamke mwingine ambaye anamtilia umuhimu zaidi kuliko mimi na watoto wangu na hunizuia mambo ambayo anamruhusu mwanamke mwingine. Hali yangu naye iko hivi. Unasemaje juu ya hilo?
Jibu: Wajibu juu ya mume ni kufanya uadilifu baina ya wake zake na wala haruhusiwi kudhulumu. Yeye ataulizwa juu ya jambo hili. Hivyo ni wajibu kwa wanaume waliooa wake zaidi ya mmoja kufanya uadilifu baina yao, wamtake msaada Allaah na wamchunge (Subhaanahu wa Ta´ala) katika kila jambo: katika kugawa zamu, katika matumizi na katika mambo ya kuwatuliza nyoyo zao na kuepuka kueneza chuki baina yao. Hivi ndivyo inavyopaswa kwa mume kuwa na hekima, ajitahidi kwa kila jambo linalotuliza hali na kurekebisha nyoyo, kuwafanya wake wawili au zaidi wawe katika raha na utulivu kwa sababu ya uadilifu wake, uangalizi wake na tabia yake njema kwao wote. Huu ndio wajibu wake.
Tunawanasihi wake pia wasaemehe baadhi ya mambo, wasiwe wakali sana na wasichunguze kila jambo. Kwa sababu mwenye kufanya ugumu atajuta na ugumu huo unaweza kuvunja familia na maisha ya ndoa isipokuwa Allaah atakavyo. Hivyo inafaa kwa wanawake pia kusamehe baadhi ya mambo na wasimkaze sana mume katika masuala ya uadilifu ikiwa ni makosa madogo au jambo dogo, kwani yanahitaji kuvumiliwa na kupuuzwa. Lazima kuwe na juhudi kutoka kwa mume na pia msamaha kutoka kwa wake katika baadhi ya mambo yanayoweza kutokea kutoka kwa mume, huenda si kwa makusudi au huenda amelazimika nayo. Basi inafaa kwa mwanamke kumsamehe baadhi ya mambo ili ipatikane maelewano na ushirikiano katika kheri.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3377/العدل-بين-الزوجات
Imechapishwa: 21/09/2026
https://firqatunnajia.com/nasaha-kwa-waume-kujitahidi-uadilifu-na-wanawake-kupuuzia-baadhi-ya-mambo/