179 – ´Amr bin ´Aliy ametukhabarisha: Mu´tamir ametuhadithia: Nimemsikia Humayd akisimulia kutoka kwa Anas, ambaye ameeleza:

“Abu Twalhah alipiga upinde mbele ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), ambapo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akajinyoosha kuangalia ni mahali gani itaangukia mishale yake. Ndipo Abu Twalhah akasema: “Hivi ndivyo, ee Mtume wa Allaah! Wazazi wangu watolewe fidia kwako. Koo langu mbele ya koo lako!”[1]

[1] Ibn Hibbaan (2250), ambaye ameisahihisha.

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 119
  • Imechapishwa: 21/09/2026