Swali: Katika mfano uliotajwa kuhusu manneo Yake Allaah (Ta´ala):
لُعِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن بَنِي إِسْرَائِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُودَ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ كَانُوا لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ
“Wamelaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa israaiyl kupitia ulimi ya Daawuud na ‘Iysaa mwana wa Maryam – hivyo ni kwa sababu ya kuasi kwao na walikuwa wakivuka mipaka. Walikuwa hawakatazani maovu waliyofanya.” (05:78-79)
Je, maana yake ni kwamba nikimkataza mtu maovu kisha asiache, basi nijiepushe kula naye na kuishi naye mpaka aache maovu yake hata kama ni maovu madogo?
Jibu: Ndiyo, hilo ni miongoni mwa adhabu za wana wa israaiyl. Mtu akimuona ndugu yake katika maovu, basi anatakiwa aendelee kumshauri na kumuongoza. Lakini asimfanye kuwa rafiki wa karibu, kikao chake na wala kushirikiana naye kula wakati bado yuko katika maovu yake. Hili ndilo lililotokea kwa wana wa israaiyl. Ajitahidi kuondoa maovu kwa nasaha na maelekezo. Ikiwa hilo halikupelekea matokeo yanayotakiwa, basi amuhame.
Suala la kuhama na kumsusia wanazuoni wana maneno matatu:
1 – Inapendeza moja kwa moja.
2 – Ni wajibu moja kwa moja.
3 – Kuna ufafanuzi; ikiwa ataona kwamba kumsusia kuna athari na kutamzuia na maovu, basi amsuse. Ikiwa ataona kwamba kumsusia kutazidisha shari yake na kumweka mbali zaidi na uongofu, basi asimsuse. Bali aendelee na nasaha na kukemea bila kumsusia.
Maoni haya ndio ya kati ndiyo yaliyo karibu zaidi na usawa kwa mujibu wa dalili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwasusia baadhi ya watu na kuwaacha wengine. Aliwasusia watu ambao aliona kususiwa kwao kuna athari, kama Ka´b bin Maalik na wenzake, kwa sababu aliona hilo litawasaidia kurejea na kuacha makosa yao.
Aliwaacha wengine kama ´Abdullaah bin Ubayy bin Saluul na baadhi ya wanafiki, kwa sababu aliona katika kuwasusia khatari kwa waislamu. Hivyo aliwaacha na akaendelea kuwafundisha na kuwashauri kwa matumaini ya kuongoka na ili waislamu wawe salama na shari yao.
Kwa hiyo wewe kwa mtu unayehusiana naye fanya hivi: ukiona kumsusia na kuacha kukaa naye na kuwasiliana naye kuna manufaa, basi fanya hivyo. Ukiona kuwasiliana naye wakati mwingine, kumtembelea wakati mwingine na kukutana naye wakati mwingine kuna karibu zaidi ya kukemea maovu na kumwongoza, basi fanya hivyo. Usimkate kabisa ikiwa unatarajia maovu yataondoka kwa njia ya kumtembelea na kwamba kumsusia kabisa kunaweza kumzidishia shari na kumweka mbali na uongofu. Tumia kile unachoona kinafaa zaidi, si kwa ajili ya dunia au matamanio yako, bali kwa ajili ya maslahi ya dini. Allaah Awape wote tawfiki na uongofu.
Swali: Hili hata ikiwa ni ndugu wa karibu?
Jibu: Ndiyo, hata kama ni ndugu wa karibu au wa mbali.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3365/حكم-هجر-من-لم-ينته-عن-المنكر
- Imechapishwa: 21/09/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3365/حكم-هجر-من-لم-ينته-عن-المنكر
Imechapishwa: 21/09/2026
https://firqatunnajia.com/maoni-matatu-ya-wanazuoni-kuhusu-kumsusa-mtenda-dhambi/