180 – ´Amr bin Yahyaa bin al-Haarith ametukhabarisha: Abu Swaalih ametukhabarisha: Abu Ishaaq ametukhabarisha, kutoka kwa Khaalid, kutoka kwa Abu Qilaabah, kutoka kwa Qabiysah bin Dhu-ayb, kutoka kwa Umm Salamah, ambaye ameeleza:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliingia kwa Abu Salamah. Macho yake yamefumbuliwa, akayafumba na kusema: “Ee Allaah! Msamehe Abu Salamah na inua ngazi yake miongoni mwa walioongoka na uwape kizazi chake kilichobakia mrithi. Tughufirie sisi na yeye, ee Mola wa walimwengu wote! Ee Allaah! Lipanua kaburi lake na umtilie nuru ndani yake.”[1]

[1] Muslim (920).

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 119
  • Imechapishwa: 22/09/2026