Swali: Unamnasihi nini kijana anayependa kuchora?

Jibu: Uchoraji umegawanyika aina mbili:

1 – Akachora mito, milima, miti, jua, mwezi, nyota na viumbe vyenginevyo visivokuwa na roho. Ni jambo linalojuzu na halina ubaya wowote.

2 – Akachora wanyama kama vile ngamia, farasi, watu na viumbe vyengine vyenye roho. Ni haramu haijuzu bali ni dhambi kubwa. Imethibiti kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani watengeneza picha. Je, unaridhia kutolewa katika rehema za Allaah? Hakuna yeyote anayeridhia jambo hilo.

Nadhani ukichora vile viumbe visivoykuwa na roho kama vile jua, mwezi, nyota, milima, mito na vyenginevyo, basi nafikiri kuwa utajiona kuwa hodari sana na utahisi furaha kubwa kwa burudani yako hii. Lazimiana na budurani yako hii na jiepushe na yale ambayo Allaah amekuharamishia. Yale ambayo Allaah amehalalishia yanawatosheleza waja kutokamana na yale aliyowaharamishia.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/352-353)
  • Imechapishwa: 21/04/2026