Kuswali kwa kuelekea Qiblah

Swali: Kikosi cha waswaliji wanaswali kwa kuelekea Qiblah cha msikiti. Je, swalah inasihi?

Jibu: Swalah ni sahihi kwa sababu ya ueneaji wa maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ardhi nzima imefanywa kwangu mimi na ummah wangu kuwa ni mahali pa kuswalia na yenye kusafisha.”[1]

Hata hivyo chooni kunaweza kuwa na harufu mbaya inayowaathiri na kuwashawishi waswaliji. Katika hali ni vyema kujiepusha kukielekea kwa sababu hii. Kwa sababu kila kitu kinachomwathiri mswaliji anatakiwa kujiepusha nacho. Siku moja ilitokea kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuswali na kanzu yenye marembo na akawa misitarimisitari yake. Alipomaliza kuswali akasema:

“Ipelekeni kanzu hii kwa Abu Jahm na mniletee Anbajaaniyah[2] ya Abu Jahm. Inanishughulisha kutokamana na swalah yangu.”[3]

Kwa sababu alitazama mara moja na jambo hilo likawa linamshughulisha kutokana na swalah. Ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaamrisha kanzu hii apewe Abu Jahm na badala yake iletwe nguo yake nyingine. Faida tunayopata kutoka katika Hadiyth hii ni kwamba kila kitu ambacho kinamshughulisha mtu kutokana na swalah yake kinatakiwa kuepukwa.

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

[2] Nguo pana ambayo haikufumwa.

[3] al-Bukhaariy, Muslim na Maalik.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/436)
  • Imechapishwa: 21/04/2026