Wapo watu wanaodhani kwamba kufanya ugumu katika mambo ya lazima na kuacha ruhusa ni katika kumcha Allaah. Mambo sivyo kabisa. Vipi iwe hivyo na hali Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
’”Msijikazie juu ya nafsi zenu ambapo Allaah atawakazia. Kwani watu fulani walijifanyia ugumu juu ya nafsi zao, basi Allaah akawafanyia ugumu. Hayo ndiyo mabaki yao katika masinagogi na makaazi yao:
وَرَهْبَانِيَّةً ابْتَدَعُوهَا مَا كَتَبْنَاهَا عَلَيْهِمْ
”Utawa wameuzusha wao wenyewe – hatukuwaandikia hayo juu yao.”[1][2]
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika Allaah anapenda zichukuliwe ruhusa Zake kama anavyopenda zichukuliwe amri Zake za lazima.”[3]
”Hakika Allaah (Ta´ala) anapenda zikubaliwe ruhusa Zake kama mja anavyopenda msamaha wa Mola wake.”[4]
”Hakika Allaah anapenda zichukuliwe ruhusa Zake kama anavyochukia kufanywa maasi Yake.”[5]
”Wameangamia wenye kupitiliza. Wameangamia wenye kupitiliza. Wameangamia wenye kupitiliza.”[6]?
Ni kweli kwamba wapo katika waja wema, wenye juhudi na bidii, ambao hawachukui isipokuwa mambo ya lazima; si kwa kuacha yaliyothibiti, wala si kwa kuichukia ruhusa iliyo halali, bali ni kwa kulea nafsi juu ya lililo bora na kuipeleka kwenye lililo kamilifu zaidi. Hili ndilo wanazuoni wa Fiqh wanaliita kuchukua tahadhari na kutoka katika nje ya tofauti kwa ajili ya kuchagua lililo na maafikiano na umoja. Msingi wake ni yale yaliyosihi katika Sunnah:
”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali usiku mpaka miguu yake inavimba.” Akaambiwa: ”Unajitaabisha hivi na hali Allaah ameshakusamehe madhambi yako yaliyotangulia na yatakayokuja baadaye?” Akasema: ”Je, nisiwe mja mwenye kushukuru?”[7]
Allaah atujaalie tuwe miongoni mwa waja Wake wenye kushukuru, atupe ufahamu katika dini, atukusanye pamoja na wale aliowaneemesha ambao ni Manabii, wakweli, mashahidi na wema. Sifa zote njema ni za Allaah, Mola wa walimwengu wote.
Nilipitia rasimu yake kisha nikairekebishe kulingana na unavyoona. Hayo yamefanyika katika Rabiy´ al-Aakhir mwaka wa 1332 Dameski, Shaam. Sifa zote njema ni za Allaah, Mwenye utukufu na ukarimu.
[1] 57:27
[2] Abu Daawuud kupitia kwa Anas (Radhiya Allaahu ´anh). (al-Qaasimiy)
[3] Ahmad kupitia kwa ´Umar na at-Twabaraaniy kupitia kwa Ibn ´Abbaas na Ibn Mas´uud. (al-Qaasimiy)
Hadiyth ni Swahiyh na imetajwa katika “Irwaa’-ul-Ghaliyl” (557).
[4] at-Twabaraaniy kupitia kwa Abud-Dardaa’, Waathilah, Abu Umaamah na Anas. (al-Qaasimiy)
Cheni yake ya wapokezi ni dhaifu, kama ilivyotajwa katika marejeo yaliyotangulia. Imetajwa katika “adh-Dhwa´iyfah” (508).
[5] Ahmad, Ibn Hibbaan na al-Bayhaqiy kupitia kwa Ibn ´Umar. (al-Qaasimiy)
Imetajwa katika marejeo yaliyotangulia na katika “Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah” (218).
[6] Muslim (2670).
[7] al-Bukhaariy (4836) na Muslim (2819).
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 75-76
- Imechapishwa: 21/04/2026

Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 75-76
Imechapishwa: 21/04/2026
https://firqatunnajia.com/51-usijifanyie-ugumu/