50. Pata mazingatio kwa Abu Haniyfah na ash-Shaafi´iy

Imetangulia kwamba al-Kaasaaniy mwishoni mwa umri wake kwamba Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah) alirejea katika maoni ya Abu Yuusuf na Muhammad kuhusu kupaka juu ya soksi. Hilo ni kwa sababu alipaka juu ya soksi zake katika maradhi yake, kisha akawaambia waliomtembelea:

”Nimefanya jambo nililokuwa nikiwakataza watu kulifanya.”

Kujirejea kwa Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah) ni katika fadhilah na uadilifu wake. Wanazuoni walibadilisha maoni kwenda katika yaliyo na nguvu na usahihi zaidi ni miongoni mwa mambo ambayo yaliwafanya kutambulika kuwa ni miongoni mwa fadhilah zao. Katika mafunzo makubwa ya kisa hiki ni kwamba imamu anajirejea na kutamka wazi kujirejea kwake. Sambamba na hilo mpinzani mkali anakataa kujirejea kwenda kweye haki hata akisomewa hoja zinazoweza kulainisha chuma na kupasua miamba. Si ajabu kabisa, kwani wanazuoni walikuwa na upole, ukamilifu, tabia njema, uadilifu na kukubali haki, mambo ambayo sifa zake zilisambaa kila mahali.

Yachukuliwe pia mazingatio kwa Imaam ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) alipohama kutoka ´Iraaq kwenda Misri na kuifanyia upya utafiti madhehebu yake ya zamani, akajirejea katika masuala mengi. Hilo limehesabiwa kuwa ni katika fadhilah zake za juu. Sababu yake ni kumcha Allaah na kuitanguliza Aakhirah, kwani uchamungu humzuia mchaji kufuata matamanio na dunia. Hivyo ndivyo alivyofanya Abu Haniyfah (Rahimahu Allaah) alipojirejea katika maoni ya kupaka juu ya soksi.

  • Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 70-71
  • Imechapishwa: 21/04/2026