Haifichiki kwamba ruhusa zilizonukuliwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni neema kubwa katika kila hali. Lakini ukamilifu wa neema ya kutungwa kwake huonekana zaidi katika baadhi ya hali, kama ruhusa ya kupangusa juu ya soksi katika siku za baridi, nyakati za safari, hali za maradhi, kupasuka kwa miguu, ukavu mkali wa ngozi ya miguu, kuvimba kwake na yanayofanana na hayo. Kama alivyowaamuru Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kikosi waliomlalamikia baridi iwapatayo kwamba wapake juu ya vilemba na vitambaa vya joto, kama tulivyotangulia kutaja. Kama alivosema Thawbaan (Radhiya Allaahu ´anh):
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alituma kikosi cha wanajeshi ambapo wakakumbwa na baridi kali. Waliporejea kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakamlalamikia ile baridi waliyokutana nayo. Ndipo akawaamuru wapake juu ya vilemba na vitambaa vya kufunika miguu.”[1]
Bwana mmoja aliyemsindikiza ‘Ikrimah (Radhiya Allaahu ´anh) kwenda Waasitw[2] amesema:
”Sikumwona akiosha miguu yake. Bali alikuwa anapangusa juu yake mpaka akatoka katika mji huo.”
Ameipokea Ibn Jariyr katika “Jaamiy´-ul-Bayaan”.
[1] Ahmad (5/277).
[2] Kwa maana wakati wa safari yake kwenda huko. Fikiria hali yake wakati wa safari yake. Safari ni kipindi cha ruhusa. Shangazwa na uelewa na ujuzi wake – Allaah awe radhi naye.
- Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 74
- Imechapishwa: 21/04/2026
Haifichiki kwamba ruhusa zilizonukuliwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni neema kubwa katika kila hali. Lakini ukamilifu wa neema ya kutungwa kwake huonekana zaidi katika baadhi ya hali, kama ruhusa ya kupangusa juu ya soksi katika siku za baridi, nyakati za safari, hali za maradhi, kupasuka kwa miguu, ukavu mkali wa ngozi ya miguu, kuvimba kwake na yanayofanana na hayo. Kama alivyowaamuru Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kikosi waliomlalamikia baridi iwapatayo kwamba wapake juu ya vilemba na vitambaa vya joto, kama tulivyotangulia kutaja. Kama alivosema Thawbaan (Radhiya Allaahu ´anh):
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alituma kikosi cha wanajeshi ambapo wakakumbwa na baridi kali. Waliporejea kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakamlalamikia ile baridi waliyokutana nayo. Ndipo akawaamuru wapake juu ya vilemba na vitambaa vya kufunika miguu.”[1]
Bwana mmoja aliyemsindikiza ‘Ikrimah (Radhiya Allaahu ´anh) kwenda Waasitw[2] amesema:
”Sikumwona akiosha miguu yake. Bali alikuwa anapangusa juu yake mpaka akatoka katika mji huo.”
Ameipokea Ibn Jariyr katika “Jaamiy´-ul-Bayaan”.
[1] Ahmad (5/277).
[2] Kwa maana wakati wa safari yake kwenda huko. Fikiria hali yake wakati wa safari yake. Safari ni kipindi cha ruhusa. Shangazwa na uelewa na ujuzi wake – Allaah awe radhi naye.
Muhusika: ´Allaamah Muhammad Jamaal-ud-Diyn bin Muhammad al-Qaasimiy (afk. 1332)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Mash ´alaal-Jawrabayn, uk. 74
Imechapishwa: 21/04/2026
https://firqatunnajia.com/49-uislamu-ni-neema-kubwa/