Swali: Ni zipi nasaha zenu kwa wale ambao hawahudhurii swalah ya Fajr pamoja na mkusanyiko?
Jibu: Ni wajibu wa muumini wa kiume na muumini wa kike kujitahidi kutekeleza swalah ndani ya wakati wake na kutojifananisha na wanafiki. Hivi ndivyo hali ya mnafiki:
”Swalah nzito zaidi kwa wanafiki ni swalah ya ´Ishaa na swalah ya Fajr.”
Ni lazima kuhadhari na kufanana nao na aamke kuswali Fajr pamoja na waislamu. Aidha familia yake wanapaswa kumwamsha mpaka aswali pamoja na waislamu. Haijuzu kuchukua wepesi katika jambo hili. Mwanamke vilevile anatakiwa kuswali ndani ya wakati. Haya yote ni wajibu na ni katika mambo muhimu kabisa. Ni lazima kuhadhari na kujifananisha na wanafiki.
Na yule anayekusudia kuiacha swalah mpaka aiswali wakati wa jua kuchomoza mtu huyo ni kafiri. Amekusudia kuiacha. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Ahadi iliyoko baina yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi yeyote atakayeiacha basi amekufuru.”
”Baina ya mtu na ukafiri na ushirikina ni kuacha swalah.”
Ni lazima kuhadhari na hilo. Ni lazima aamshwe na kuweka saa juu ya wakati ili aswali pamoja na waislamu na aswali swalah ndani ya wakati wake. Mwanamke vilevile anapasa kujitahidi mpaka aswali swalah ndani ya wakati wake. Ni mamoja iwe Fajr na swalah nyenginezo. Tunamuomba Allaah awape wote uongofu na usalama.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31767/ما-النصيحة-لمن-لا-يحضر-صلاة-الفجر
- Imechapishwa: 30/11/2025
Swali: Ni zipi nasaha zenu kwa wale ambao hawahudhurii swalah ya Fajr pamoja na mkusanyiko?
Jibu: Ni wajibu wa muumini wa kiume na muumini wa kike kujitahidi kutekeleza swalah ndani ya wakati wake na kutojifananisha na wanafiki. Hivi ndivyo hali ya mnafiki:
”Swalah nzito zaidi kwa wanafiki ni swalah ya ´Ishaa na swalah ya Fajr.”
Ni lazima kuhadhari na kufanana nao na aamke kuswali Fajr pamoja na waislamu. Aidha familia yake wanapaswa kumwamsha mpaka aswali pamoja na waislamu. Haijuzu kuchukua wepesi katika jambo hili. Mwanamke vilevile anatakiwa kuswali ndani ya wakati. Haya yote ni wajibu na ni katika mambo muhimu kabisa. Ni lazima kuhadhari na kujifananisha na wanafiki.
Na yule anayekusudia kuiacha swalah mpaka aiswali wakati wa jua kuchomoza mtu huyo ni kafiri. Amekusudia kuiacha. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Ahadi iliyoko baina yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi yeyote atakayeiacha basi amekufuru.”
”Baina ya mtu na ukafiri na ushirikina ni kuacha swalah.”
Ni lazima kuhadhari na hilo. Ni lazima aamshwe na kuweka saa juu ya wakati ili aswali pamoja na waislamu na aswali swalah ndani ya wakati wake. Mwanamke vilevile anapasa kujitahidi mpaka aswali swalah ndani ya wakati wake. Ni mamoja iwe Fajr na swalah nyenginezo. Tunamuomba Allaah awape wote uongofu na usalama.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31767/ما-النصيحة-لمن-لا-يحضر-صلاة-الفجر
Imechapishwa: 30/11/2025
https://firqatunnajia.com/nasaha-kwa-anayekosa-fajr-kwa-mkusanyiko/