Napendezwa sana na kisa cha mmoja wa watu wema, naye ni Shaykh Thaaniy al-Mansuur (Rahimahu Allaah) kutoka mji wa al-Jubayl katika mkoa wa mashariki mwa Saudi Arabia. Nilikisikia kutoka kwa aliyekisikia moja kwa moja kutoka kwake na mukhtaswari wake ni huu:
Aliwahi kuitembelea nchi moja ambayo baadhi ya watu wake wamepatwa na fitina ya kujenga juu ya makaburi na kuchupa mipaka kwa watu wake. Akiwa huko alikutana na kundi la watu ndani ya msikiti mmoja uliokuwa na kaburi. Wakamsema yeye na watu wa nchi yake kuwa hawampendi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Akawajibu na kuwauliza: “Je, katika nchi yenu kuna baa za pombe na maeneo ya uasherati na ufuska?” Wakasema: “Ndiyo, yapo mengi!” Akasema: “Nchini mwetu hakuna hata sehemu moja kama hiyo.” Kisha akawaambia: “Nini hukumu ya kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika swalah kwenu?” Wakasema: “Inapendeza.” Akasema: “Kwetu sisi ni nguzo ya swalah; mswaliji asipoisoma basi swalah yake haisihi.” Kisha akauliza: “Basi nani anayestahiki zaidi kuonekana kuwa anampenda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?”
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 83
- Imechapishwa: 27/05/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket