Namna ya usafishaji wa matone ya mkojo yaliyompata mtu

Swali: Ikiwa mtu atatokwa na mkojo na akataka kutawadha tena, je, matone ya mkojo yanayomfikia ni twahara au anatakiwa kulowanisha mkono wake kwa maji na kuyapangusa?

Jibu: Mkojo ni najisi. Kwa hiyo ikiwa kilichompata mtu ni matone ya mkojo basi ni wajibu kwake kuosha sehemu ya mwili au nguo yake iliyofikiwa na matone hayo. Haitoshelezi kuitwaharisha kwa kuipangusa kwa maji. Hukumu ni hiyohiyo ikiwa matone hayo ni ya maji ambayo aliyamimina juu ya mkojo.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/235)
  • Imechapishwa: 06/11/2026