Swali: Ikiwa mtu anataka kutawadha kwa ajili ya swalah, je, inatosha kumimina maji juu ya kiungo mara moja, kisha kuyapitisha kwa kupangusa sehemu iliyobaki ya kiungo hicho? Je, inatosha kuosha kila kiungo mara moja na kisha kuswali?
Jibu: Inatosha kwa mwenye kutawadha kumimina maji juu ya kila kiungo miongoni mwa viungo vinavyopaswa kuoshwa katika wudhuu´, kwa sharti kwamba maji yafike sehemu yote ya kiungo hicho. Ama kuosha mara ya pili na ya tatu ni Sunnah tu. Hata hivyo ikiwa mara moja ya kuosha hakukufikisha maji kwenye sehemu yote ya kiungo, haitoshelezi katika wudhuu´, hata ikiwa mtu atapangusa sehemu iliyobaki kwa maji.
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/237)
- Imechapishwa: 06/11/2026
Swali: Ikiwa mtu anataka kutawadha kwa ajili ya swalah, je, inatosha kumimina maji juu ya kiungo mara moja, kisha kuyapitisha kwa kupangusa sehemu iliyobaki ya kiungo hicho? Je, inatosha kuosha kila kiungo mara moja na kisha kuswali?
Jibu: Inatosha kwa mwenye kutawadha kumimina maji juu ya kila kiungo miongoni mwa viungo vinavyopaswa kuoshwa katika wudhuu´, kwa sharti kwamba maji yafike sehemu yote ya kiungo hicho. Ama kuosha mara ya pili na ya tatu ni Sunnah tu. Hata hivyo ikiwa mara moja ya kuosha hakukufikisha maji kwenye sehemu yote ya kiungo, haitoshelezi katika wudhuu´, hata ikiwa mtu atapangusa sehemu iliyobaki kwa maji.
Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/237)
Imechapishwa: 06/11/2026
https://firqatunnajia.com/hapa-ndipo-itatosha-kumimina-maji-kwenye-viungo-vya-mwili/