Swali: Ni ipi sifa ya kuswali swalah ya kujitolea juu ya kipando katika wakati huu?

Jibu: Anaswali juu ya kipando, anasoma huku akiwa amekaa, anarukuu huku akiwa amekaa hewani na anasujudu huku akiwa amekaa hewani, kama Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alivyokuwa akifanya safarini. Hivi hivi ndivyo inavyokuwa katika gari, katika treni, katika ndege na katika merikebu. Lakini akipata uwezo wa kusujudu ndani ya gari, treni, merikebu au ndege – ikiwa yupo sehemu yenye nafasi na anaweza kusujudu na kusimama – basi atafanya hivyo katika swalah ya faradhi tu. Ama swalah inayopendeza inajuzu kuswali huku amekaa, kwa sababu katika swalah ya kujitolea kusimama si wajibu. Lakini anayeswali akiwa amekaa hupata nusu ya thawabu ya anayeswali akiwa amesimama katika swala ya kujitolea. Ama swalah ya faradhi ni lazima aswali akiwa amesimama. Ikiwa kunayo haja ya kuswali ndani ya ndege, kwa namna ya kwamba muda umeingia na yuko ndani ya ndege, ndani ya merikebu au ndani ya gari na muda umeingia, basi ataswali kulingana na hali yake. Lakini katika gari anaweza kusimamisha gari na kuswali ardhini, kama ilivyo kwa kipando. Ama ndani ya ndege hana njia nyingine. Kwa hiyo akikhofia kupitwa na muda ataswali ndani yake kwa upande wa mwelekeo wa Qiblah kulingana na mwendo wa ndege na ataswali akiwa amekaa:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

[1] 64:16

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31699/ما-صفة-صلاة-النافلة-على-الراحلة
  • Imechapishwa: 04/12/2025