Swali: Ni ipi Sunnah katika kupanga safu za waswaliji? Je, mwenye kuswali aache kati ya mguu wake nafasi ya vidole vinne au aambatanishe mguu wake na wa aliye pembeni yake?
Jibu: Sunnah ni kusogeleana katika safu na kutoacha nafasi yoyote kati ya miguu. Mguu wa mwenye kuswali uwe umeambatana na mguu wa mwenzake bila kusababisha madhara, bila kusuguana wala kuleta madhara. Bali amkaribie mguu wake kwa mguu wa mwenzake wala asisimame kwa kujitanua kupita kiasi. Baadhi ya watu hujitanua na kuchukua nafasi ya watu wawili, jambo hili halifai. Bali kila mmoja amsogelee mwenzake mpaka wazibe pengo. Kwa sababu hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Sawazisheni, zibenzeni mapengo, zibeni nafasi zilizo wazi na wala msiache mapengo kwa shaytwaan.”
Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Mtu alikuwa akiambatanisha mguu wake na mguu wa mwenzake.”
Kwa maana walikuwa wanaziba mapengo. Maana yake si kwamba mtu amsugue au amuumeze mwenzake, hapana. Mtu hasuguani mguu kwa mguu kwa kuumizana, bali anaambatanisha ili pasiwe na pengo kati yao.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/122)
- Imechapishwa: 02/03/2026
Swali: Ni ipi Sunnah katika kupanga safu za waswaliji? Je, mwenye kuswali aache kati ya mguu wake nafasi ya vidole vinne au aambatanishe mguu wake na wa aliye pembeni yake?
Jibu: Sunnah ni kusogeleana katika safu na kutoacha nafasi yoyote kati ya miguu. Mguu wa mwenye kuswali uwe umeambatana na mguu wa mwenzake bila kusababisha madhara, bila kusuguana wala kuleta madhara. Bali amkaribie mguu wake kwa mguu wa mwenzake wala asisimame kwa kujitanua kupita kiasi. Baadhi ya watu hujitanua na kuchukua nafasi ya watu wawili, jambo hili halifai. Bali kila mmoja amsogelee mwenzake mpaka wazibe pengo. Kwa sababu hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Sawazisheni, zibenzeni mapengo, zibeni nafasi zilizo wazi na wala msiache mapengo kwa shaytwaan.”
Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Mtu alikuwa akiambatanisha mguu wake na mguu wa mwenzake.”
Kwa maana walikuwa wanaziba mapengo. Maana yake si kwamba mtu amsugue au amuumeze mwenzake, hapana. Mtu hasuguani mguu kwa mguu kwa kuumizana, bali anaambatanisha ili pasiwe na pengo kati yao.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/122)
Imechapishwa: 02/03/2026
https://firqatunnajia.com/namna-ya-kupanga-safu/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket