Swali: Amesema:
”Anatangulizwa mbele mkubwa zaidi kisha aliyetangulia.”
Kwa maana katika swalah ya jeneza. Je, yule bora zaidi awekewe upande wa Qiblah na yule wa daraja ya chini awe upande wa imamu au kinyume chake?
Jibu: Kilichojulikana ni kwamba wanaume hutangulizwa, kisha watoto wa kiume, kisha wanawake katika kuswaliwa kwa jeneza karibu na imamu. Hivi ndivyo maandiko yalivyoonyesha. Mwanzo kabisa ni wanaume, kisha watoto wa kiume, kisha wanawake ambao huwekwa upande wa Qiblah. Aliye bora zaidi huwa karibu na imamu; wanaume kwanza, kisha watoto wa kiume karibu na imamu, nyuma yao upande wa Qiblah ni wanawake. Hayo ndiyo mafunzo yaliyopendekezwa. Vivyo hivyo katika safu za swalah: safu za mbele ni za wanaume, kisha watoto wa kiume, kisha wanawake nyuma yao.
Swali: Hatukuelewa vizuri maelezo haya. Ikiwa kuna wanaume na wanawake, tunawaweka vipi?
Jibu: Jeneza la mwanamume linawekwa karibu zaidi na imamu. Kisha nyuma yake (kwa mbali zaidi na imamu) huwekwa jeneza la mtoto wa kiume, kisha upande wa Qiblah huwekwa jeneza la mwanamke.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1030/كيفية-وضع-الجناىز-عند-الصلاة-عليها
- Imechapishwa: 13/01/2026
Swali: Amesema:
”Anatangulizwa mbele mkubwa zaidi kisha aliyetangulia.”
Kwa maana katika swalah ya jeneza. Je, yule bora zaidi awekewe upande wa Qiblah na yule wa daraja ya chini awe upande wa imamu au kinyume chake?
Jibu: Kilichojulikana ni kwamba wanaume hutangulizwa, kisha watoto wa kiume, kisha wanawake katika kuswaliwa kwa jeneza karibu na imamu. Hivi ndivyo maandiko yalivyoonyesha. Mwanzo kabisa ni wanaume, kisha watoto wa kiume, kisha wanawake ambao huwekwa upande wa Qiblah. Aliye bora zaidi huwa karibu na imamu; wanaume kwanza, kisha watoto wa kiume karibu na imamu, nyuma yao upande wa Qiblah ni wanawake. Hayo ndiyo mafunzo yaliyopendekezwa. Vivyo hivyo katika safu za swalah: safu za mbele ni za wanaume, kisha watoto wa kiume, kisha wanawake nyuma yao.
Swali: Hatukuelewa vizuri maelezo haya. Ikiwa kuna wanaume na wanawake, tunawaweka vipi?
Jibu: Jeneza la mwanamume linawekwa karibu zaidi na imamu. Kisha nyuma yake (kwa mbali zaidi na imamu) huwekwa jeneza la mtoto wa kiume, kisha upande wa Qiblah huwekwa jeneza la mwanamke.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1030/كيفية-وضع-الجناىز-عند-الصلاة-عليها
Imechapishwa: 13/01/2026
https://firqatunnajia.com/namna-ya-kupanga-maiti-waliochanganyika-waume-kwa-wake-2/