Namna ya kuondoa misalaba inayokuwa katika vitu

Swali: Baadhi ya magari yanakuwa na misalaba.

Jibu: Misalaba hiyo isuguliwe na kuondolewa pia.

Swali: Hata kwenye sofa pia?

Jibu: Kitu kinachokanyagwa jambo lake ni sahali. Lakini kama ni rahisi ausugue. Vinginevyo bora auondoe.

Swali: Ikiwa si rahisi hapati dhambi?

Jibu: Itwezwe ardhini. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa akiona msalaba wowote isipokuwa anaukata.”

Bi maana anauvunja. Anaweza kuusugua msalaba huo na akaweka juu yake kitambara au kitu kingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22144/ماذا-يفعل-من-لديه-سيارة-فيها-صلبان
  • Imechapishwa: 29/10/2022