Swali: Ni vipi nimtendee mama yangu wema baada ya kufa kwake?

Jibu: Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba aliulizwa na mtu ambaye alisema: “Ee Mtume wa Allaah! Kumebaki kitu katika kuwatendea wema wazazi wangu ninachoweza kuwatendea baada ya kufa kwao?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kuwaombea du´aa, kuwaombea msamaha, kuwatimizia ahadi zao, kuwakirimu marafiki zao, kuwaunga jamaa zao wa lazima.”

Yote haya ni katika kuwatendea wema wazazi baada ya kufa kwao.

Kwa hivyo tunakuusia kuwaombea du´aa, msamaha na kutekeleza wasia wa mama yako unaokubaliki katika Shari´ah. Aidha wakirimu marafiki zake, waunge wajomba, shangazi na jamaa zako wengine upande wa mama yako.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ajmuu´-ul-Fataawaa (09/295)
  • Imechapishwa: 17/07/2021