Namna ya kumsalimia Mtume wakati wa kutembelea kaburi lake

Swali: Wakati wa kutembelea msikiti wa Mtume, je, imependekezwa kutembelea kaburi na kumsalimia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), pamoja na kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Niswalieni, kwani hakika du´aa yenu hunifikia popote mlipo.”

Ni ipi dalili ya kwamba hilo limesuniwa?

Jibu: Sunnah kwa mwenye kuutembelea msikiti wa Mtume ni kuswali humo Rak´ah mbili, kisha baada ya hapo kulitembelea kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuwasalimia Maswahabah wake wawili. Wakati anapofunga safari na kusafiri, nia yake iwe ni kuutembelea msikiti. Atakapofika msikitini, aswali humo Rak´ah mbili, kisha baada ya hapo alitembelee kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa sababu katika hali hii hakusafiri wala kufunga safari kwa ajili ya kaburi.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
  • Imechapishwa: 25/09/2026