Swali: Mwanamke mjamzito alijilazimisha katika siku moja alipokuwa akifanya kazi jikoni, akainama sana kwa nguvu, kisha akahisi mtoto tumboni akisogea kwa hali isiyo ya kawaida. Wakati wa kujifungua, mtoto alizaliwa akiwa amekufa. Hajui ikiwa kifo cha mtoto kilitokana na kujilazimisha huko au hapana. Je, kuna jambo lolote linalomlazimu?
Jibu: Ikiwa anayo dhana kubwa ya kwamba alifanya hivyo kwa makusudi na kwamba mtoto alikufa kwa sababu ya kujilazimisha huko na kuinama huko, basi analazimika kutoa kafara na pia analazimika kutoa fidia. Kafara ni kumkomboa mtumwa. Asipopata, basi afunge miezi miwili mfululizo. Aidha analazimika kutoa diyah kwa baba yake, nayo ni kumkomboa mtumwa wa kiume au wa kike – ikiwa baba yake yuko hai – au kwa ndugu zake. Naye harithi chochote kutoka kwake, kwa sababu yeye ndiye aliyesababisha kifo chake.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
- Imechapishwa: 25/09/2026
Swali: Mwanamke mjamzito alijilazimisha katika siku moja alipokuwa akifanya kazi jikoni, akainama sana kwa nguvu, kisha akahisi mtoto tumboni akisogea kwa hali isiyo ya kawaida. Wakati wa kujifungua, mtoto alizaliwa akiwa amekufa. Hajui ikiwa kifo cha mtoto kilitokana na kujilazimisha huko au hapana. Je, kuna jambo lolote linalomlazimu?
Jibu: Ikiwa anayo dhana kubwa ya kwamba alifanya hivyo kwa makusudi na kwamba mtoto alikufa kwa sababu ya kujilazimisha huko na kuinama huko, basi analazimika kutoa kafara na pia analazimika kutoa fidia. Kafara ni kumkomboa mtumwa. Asipopata, basi afunge miezi miwili mfululizo. Aidha analazimika kutoa diyah kwa baba yake, nayo ni kumkomboa mtumwa wa kiume au wa kike – ikiwa baba yake yuko hai – au kwa ndugu zake. Naye harithi chochote kutoka kwake, kwa sababu yeye ndiye aliyesababisha kifo chake.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (25)
Imechapishwa: 25/09/2026
https://firqatunnajia.com/amemuua-mtoto-alipokuwa-jikoni-anapika/