Namna ya kumsalimia mama yangu makaburini

Swali: Mmoja wa ndugu anasema kuwa anataka kumzuru mama yake kaburini na anauliza ni vipi atamsalimia? Je, niseme:

السلام عليك يا أمي

”Amani iwe juu yako, ee mama yangu.”

au maneno yanayofanana na hayo?

Jibu:

السلام عليكم ورحمة الله وبركاته، غفر الله لك، ورحمك، وأسكنك الجنة

”Amani iwe juu yenu na rehema za Allaah na baraka Zake, Allaah akusamehe, akurehemu na akuingize Peponi.”

na maneno mengine yanayofanana na hayo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25237/ما-كيفية-السلام-على-الميت-في-قبره
  • Imechapishwa: 22/02/2025