Swali: Je, yule mwenye kujiunga pamoja na imamu ilihali amerukuu anatakiwa kuleta Takbiyr moja au mbili?

Jibu: Anatakiwa kuleta Takbiyr-ul-Ihraam ilihali amesimama. Baada ya hapo alete Takbiyr ya kwenda katika Rukuu´ na kuinama. Ikiwa hatowahi basi inatosha kuleta Takbiyrat-ul-Ihraam. Lakini kwa sharti alete Takbiyr-ul-Ihraam na huku amesimama. Ama akileta Takbiyr-ul-Ihraam ilihali ameinama basi swalah yake ya faradhi inageuka kuwa ya sunnah. Haya ni mambo muhimu ambayo inatakiwa kuyatilia umuhimu na kutanabahi nayo.

Kilichowekwa katika Shari´ah ni kwamba akifika na akamkuta imamu yuko katika Rukuu´ basi alete Takbiyr-ul-Ihraam hali ya kusimama sawasawa. Kisha baada ya hapo ainame kwenda katika Rukuu´ baada ya kupiga Takbiyr nyingine au pasi na kuleta Takbiyr. Akipiga Takbiyr-ul-Ihraam ilihali tayari amekwishainama basi swalah yake ya faradhi inageuka kuwa ya sunnah na wala haisihi. Kwa sababu inasihi kuswali swalah ya sunnah ilihali umeketi. Kuhusu swalah ya faradhi ni lazima kwa mtu kusimama midhali mtu ana uwezo wa kufanya hivo. Yule aliyekuja amechelewa amebakiwa na Takbiyr-ul-Ihraam ambayo ni lazima kwanza ailete katika hali ya kusimama. Akipiga Takbiyr-ul-Ihraam ilihali tayari kishainama basi swalah yake ya faradhi inageuka kuwa ya sunnah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (04) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191047#191047
  • Imechapishwa: 03/09/2018