Swali: Ni vipi mtu ataharibu sanamu? Je, inatosha kuharibu uso peke yake?

Jibu: Kwa kuondosha kichwa chake. Kuliharibu kwake ni kwa kuondosha kichwa chake. Vivyo hivyo hizi picha za kisasa zinazotundikwa ima zikaharibiwa kwa kuondoshwa kichwa chake au kwa kuzitupa na kuzitweza.

Swali: Muislamu yeyote anaweza kuharibu sanamu?

Jibu: Huku ni kukataza kwa kutumia mkono. Haya yanakuwa kwa yule aliyeshika utawala mikononi. Ambaye hana utawala hawezi kufanya hivi. Haya ni kwa watawala.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (92) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/%D8%A5%D8%BA%D8%A7%D8%AB%D8%A9%20%D8%A7%D9%84%D9%84%D9%87%D9%81%D8%A7%D9%86%20%D9%85%D9%86%20%D9%85%D8%B5%D8%A7%D8%A6%D8%AF%20%D8%A7%D9%84%D8%B4%D9%8A%D8%B7%D8%A7%D9%86-29-07-1439%D9%87%D9%80%200010.mp3
  • Imechapishwa: 20/07/2018