Swali: Miaka mitatu sasa nagawanya nyama ya Udhhiyah mafungu matatu:

1 – Mafukara na masikini.

2 – Tunapika theluthi mbili nyingine nyumbani na tunakusanyika pamoja na jamaa wengine.

Je, tuna kosa katika kufanya hivo?

Jibu: Udhhiyah ni jambo Allaah amewawekea katika Shari´ah waja Wake (Subhaanahu wa Ta´ala) na amejaalia kuwa ni ´ibaadah wanayojikurubisha kwayo mbele Yake katika sikukuu ya kuchinja katika miji na mashambani. Hakuweka mpaka (Subhaanah) wa kile kiwango anachotakiwa kuchukua mchinjaji na anachotakiwa kuwapa mafukara. Amesema (Subhaanah):

فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْبَائِسَ الْفَقِيرَ

“Basi kuleni humo na lisheni ambaye ni fakiri mno.”[1]

Aayah nyingine inasema:

فَكُلُوا مِنْهَا وَأَطْعِمُوا الْقَانِعَ وَالْمُعْتَرَّ

“Kuleni kutoka humo na lisheni waliokinai.”[2]

Kilichosuniwa kwa muumini katika Udhhiyah yake ni yeye ale na alishe sehemu yake. Hapana neno na wala hapana vibaya akitoa swadaqah ya theluthi moja kuwapa mafukara na yeye akala theluthi mbili na familia yake. Inatosha pia endapo atatoa kidogo chini ya theluthi moja. Ni sawa pia akiwapa mafukara katika majirani na jamaa zake. Jambo ni lenye wasaa.

[1] 22:28

[2] 22:36

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4439/ما-المشروع-في-توزيع-الاضحية
  • Imechapishwa: 13/06/2024