Swali: Ni ipi njia ya Kishari´ah ya kumnasihi baba na kumkataza maovu? Kumkataza kwa ushupavu kunapingana na kumtendea wema?

Jibu: Kuwa na njia ya upole. Kuwa na usulubu mzuri. Zungumza nae kwa hekima na maneno mazuri. Fanya nae upole. Huenda Allaah akamwongoza. Nyinyi mnasoma mazungumzo ya Ibraahiym na baba yake:

يَا أَبَتِ

“Ee baba yangu!” (19:42)

يَا أَبَتِ

“Ee baba yangu!” (19:43)

يَا أَبَتِ

“Ee baba yangu!” (19:44)

Alifanya hivo kwa kumfikiria. Kuwa mpole kwake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (42) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2011%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 14/03/2017