Namna ambavyo mwenye hedhi atatafuta usiku wa Qadar

Swali: Ni vipi mwanamke ambaye ana udhuru wa ki-Shari´ah atasimamisha usiku wa Qadar?

Jibu: Kwa kuomba du´aa, kufanya Dhikr na kusoma Qur-aan. Hakuna ubaya kwake kufanya hivo. Nadhani kuwa una uhakika wa kutokuweko machukizo kwa mwanamke mwenye hedhi kusoma Qur-aan.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 181
  • Imechapishwa: 03/07/2022