Najisi sehemu ambayo mtu hajui ni wapi

Swali: Ikiwa najua fika kwamba sehemu fulani kuna najisi lakini nashindwa kulenga ni wapi. Nisafishe vipi?

 Jibu: Safishe sehemu hiyo yote. Ikiwa unajua kwamba nguo imepatwa na najisi lakini hujui ni wapi, ioshe nguo yote. Ikiwa unajua kuwa sehemu fulani kumepatwa na najisi lakini hujui ni wapi, paoshe pote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (86) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/NEW.lite_.mp3
  • Imechapishwa: 11/07/2018