Najisi iliyoingia ndani ya maji chini ya Qullatayn

Swali: Maji yananajisika yanapoingiwa ni madogo chini ya Qullatayn?

Jibu: Kuna makinzano yanayotambulika:

1 – Wako wanazuoni wanaosema kuwa maji yananajisika ijapo hayakubadilika.

2 – Wengine wamesema kuwa hayawi najisi isipokuwa yanapobadilisha rangi, harufu na ladha yake.

Isipokuwa yakiwa ni kidogo, kama maji ya vyombo, basi humwagwa kama vile Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alivyoamrisha kumwaga maji ya ndani ya chombo yaliyorambwa na mbwa. Mara nyingi maji madogo kama haya yanaathiriwa na najisi kwa sababu ni madogo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24683/حكم-نجاسة-الماء-اذا-كان-اقل-من-قلتين
  • Imechapishwa: 25/11/2024