Mzee anashindwa kwenda kuswali msikitini

Swali: Mwanaume mzee analalamika kuhusu miguu yake kwa kuwa haimsaidii kubeba mwili wake kwenda kuswali swalah ya mkusanyiko msikitini kutokana na ugumu wa kushuka ngazi za nyumba na mashaka ya njia. Zaidi ya hayo, hawezi kuswali akiwa amesimama, bali huswali akiwa amekaa kwenye kiti kilichoandaliwa kwa ajili ya swalah. Je, ana ruhusa ya kuswali nyumbani?

Jibu: Ikiwa hali ni kama ilivyotajwa, basi hapana vibaya kwake kuswali nyumbani kwa sababu ya udhuru huo uliotajwa. Aidha anatakiwa kusujudu chini ardhini ikiwa anaweza. Ikiwa hawezi, basi hakuna tatizo kusujudu kwa kuashiria na sujuud yake iwe chini zaidi kuliko Rukuu´ yake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/112)
  • Imechapishwa: 01/03/2026