Swali: Ni upi usahihi wa Hadiyth inayosema:
“Yeyote anayemuosha muislamu na kuficha aibu zake, hutoka katika madhambi yake kama siku aliyozaliwa na mama yake.”?
Je, katika swalah ya jeneza ni lazima kusoma du´aa ya kufungua swalah au si lazima?
Jibu: Sijui kama Hadiyth hii ina msingi wowote. Hadiyth isemayo:
“Yeyote anayemuosha muislamu na kuficha aibu zake, hutoka katika madhambi yake kama siku aliyozaliwa na mama yake.”
Siijui kuwa ina msingi wowote. Lakini inapendeza kumsitiri maiti na kutofichua chochote kibaya kinachoonekana wakati wa kumuosha. Mwoshaji inapendeza kwake awasitiri watu, aonyeshe mazuri yao na afiche mabaya yao. Hivi ndivyo wanazuoni walivyotaja. Aidha ni jambo limepokelewa katika baadhi ya Hadiyth dhaifu. Sunnah ni kwamba mwoshaji afiche kile kinachomkera au kinachoonekana kuwa ni makosa ya maiti na asikibainishe, kwa sababu kufanya hivyo ni aina ya usengenyi. Lakini akiona nuru au akiona jambo jema, anaweza kuyabainisha.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1130/الحكم-على-حديث-من-غسل-مسلما-وستر-عيبه
- Imechapishwa: 31/01/2026
Swali: Ni upi usahihi wa Hadiyth inayosema:
“Yeyote anayemuosha muislamu na kuficha aibu zake, hutoka katika madhambi yake kama siku aliyozaliwa na mama yake.”?
Je, katika swalah ya jeneza ni lazima kusoma du´aa ya kufungua swalah au si lazima?
Jibu: Sijui kama Hadiyth hii ina msingi wowote. Hadiyth isemayo:
“Yeyote anayemuosha muislamu na kuficha aibu zake, hutoka katika madhambi yake kama siku aliyozaliwa na mama yake.”
Siijui kuwa ina msingi wowote. Lakini inapendeza kumsitiri maiti na kutofichua chochote kibaya kinachoonekana wakati wa kumuosha. Mwoshaji inapendeza kwake awasitiri watu, aonyeshe mazuri yao na afiche mabaya yao. Hivi ndivyo wanazuoni walivyotaja. Aidha ni jambo limepokelewa katika baadhi ya Hadiyth dhaifu. Sunnah ni kwamba mwoshaji afiche kile kinachomkera au kinachoonekana kuwa ni makosa ya maiti na asikibainishe, kwa sababu kufanya hivyo ni aina ya usengenyi. Lakini akiona nuru au akiona jambo jema, anaweza kuyabainisha.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1130/الحكم-على-حديث-من-غسل-مسلما-وستر-عيبه
Imechapishwa: 31/01/2026
https://firqatunnajia.com/mwoshaji-kuficha-aibu-za-maiti/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket