Mwokotaji anashurutisha apewe zawadi

Swali: Kuna mtu ameokota pesa 10,000 SAR na akazitangaza. Baada ya kutimia mwaka akapatikana mwenye nazo, ambapo mwokotaji akakataa kumpa nazo mpaka ampe 1000 SAR. Je, yanafaa maombi haya?

Jibu: Ni haramu kwake. Haijuzu kwake. Ampe pesa zake. Mmiliki baadaye akimpa chochote kwa kutaka mwenyewe, hapana vibaya. Hata hivyo mwokotaji asishurutishe kupewa chochote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (44)
  • Imechapishwa: 12/07/2024